DARASA LA KUUKULIA WOKOVU
Utangulizi:
a. Maana ya Imani: Waebrania 11 : 1
-
Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo,
ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
-
Lile jambo unalolitaka ukiliweka bayana, unalipa
asilimia zote za kulifanikisha
b. Chanzo cha Imani: Warumi 10 : 17
-
Imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja
kwa Neno la Kristo
-
Kwa hiyo, unaposikiliza Neno la Kristo kwa njia
yoyote ile (inaweza kuwa kwa njia ya mahubiri au kwa kusoma Biblia n.k) imani inajengeka
ndani yako juu ya Mungu.
-
Ndani yako kwa kupitia Neno la Mungu unapata
uhakika ya kuwa Mungu yupo na anauweza wote.
-
Ili uweze kuongezeka viwango vyako vya kiroho ni
lazima uinue viwango vyako vya kumtafuta Mungu kwa njia ya Neno na Maombi, na
kuishi maisha masafi ndipo imani yako juu ya Mungu itaongezeka
Mfano: unaweza kuamini kuwa Mungu anaponya lakini usiamini
kuwa anafufua wafu. Ni muhimu kujikita sana kwenye neno lake ukamjua Mungu
zaidi
Mithali 2 : 1 – 5
-
Ukiwa ni mtu wa kusoma Neno la Mungu na
kulitafakari kila siku basi utakuwa na maisha masafi.
-
Ukijaa neno la Mungu ndani yako utaongozwa na
Roho Mtakatifu katika kutenda yale yanayompendeza Mungu siku zote. Zaburi 119 : 105
-
Neno la Mungu linatupa furaha tunapopita katika
taabu. Zaburi 119 : 92
c. Kulinda imani
i.
Dhambi inapingana na imani, maana watendao
dhambi ni wa Ibilisi na Ibilisi hawezi kukuruhusu umwamini Yesu Kristo, hivyo
basi ukitaka kutembea katika imani ya Kristo ni lazima ujifunze kuishi maisha
matakatifu. Epuka dhambi
Yohana 8 : 44
Filipi 2 : 14 – 16
Kolosai 3 : 8 – 10
ii.
Jitahidi kuwa muombaji kila wakati, imani yako
haitayumbishwa
Mathayo 17 : 21 na Marko 9 : 29
-
Hapa maombi hayakuongezei imani bali yanaondoa
hali ya kutokuamini ndani yako. Kumbuka kinachokupa imani si maombi bali ni
kusikia neno la Kristo. Hivyo maombi yanashughulikia kuondoa hali ya kutoamini
ndani ya moyo wako.
-
Na mara nyingi hiyo hali ya kutokuamini
inasababishwa na upungufu wa Neno la Mungu ndani ya moyo wa mtu.
UMUHIMU WA IMANI
1. Imani inatupa ushindi
Ushindi dhidi ya vita vya adui shetani,
magonjwa, majaribu
Ayubu
42 : 10 – 12
Isaya
38 : 5
2. Imani inaleta uponyaji kwa wenye magonjwa
na wadhaifu
Mathayo
9 : 27 – 29
Marko
2 : 4 – 5
Marko
5 : 25 – 34
Luka
5 : 17 – 26
Isaya
38 : 1 – 6
3. Imani inatutia nguvu-
Ukiwa na imani unapata nguvu ya kuvuka hata
katika magumu. Mungu anakuvusha salama
Isaya
40 : 31 – wamngojao Bwana maana yake wenye imani kuwa Yesu atarudi tena,
Mungu anawajaza nguvu za kuendelea kumtumikia kwa juhudi na kwa bidii bila
kukata tamaa wakiwa katika dunia hii iliyojaa dhiki na taabu nyingi.
4. Imani inatusaidia kuwaleta wenye dhambi kwa
Yesu.
Ukiwa na imani kubwa kiasi cha kutenda
miujiza basi watu watakapoona hayo watakubali kumpokea Yesu Kristo kwenye
maisha yao.
Matendo
11 : 24
5. Imani hutuletea amani.
Warumi
5 : 1
Isaya
36 : 1, 14 – 22; - 37 : 33 – 35
6. Imani hutupa uvumilivu.
Ukiwa na imani unaweza ukavumilia na kustahimili
changamoto unazopitia katika maisha yako
Yakobo
1 : 3 – 4
Ayubu 42
: 1 - 17
No comments:
Post a Comment