Lengo la somo: kukuwekea msukumo ndani yako wa kuendelea kuomba bila kukata tamaa ili kujiongezea akiba zaidi ya maombi mbele za Mungu.
Utangulizi:
Mbele za Mungu hakuna maombi ya watakatifu yanayopotea.
-
Mahitaji yako au majibu ya maombi yako yanategemea
kiwango cha maombi unachokiachilia ili kushughulikia mahitaji hayo. Kama hitaji
lako ni kubwa na linahitaji kiwango kikubwa cha maombi basi ujue ukiomba kwa
kiwango kidogo hakitaweza kutengeneza majibu ya maombi hayo,
-
Lakini pia unapokuwa ni muombaji wa mara kwa mara basi
ujue kuwa unajiwekea akiba ya maombi yatakayoweza kukusaidia wakati wa uhitaji.
Matendo 10
: 1 – (4) – 8
-
Hizi ni habari za mtu mmoja aliyeitwa Kornelio,
alikuwa ni kamanda wa jeshi la Kirumi lakini alikuwa ni mcha Mungu maana yake
alikuwa na hofu ya Mungu ndani yake pamoja na nyumba yake yote.
-
Kitu cha pekee kumuhusu huyu mtu ni kwamba alikuwa
anawapa watu sadaka nyingi na pia alikuwa ni muombaji. Biblia inasema siku moja
malaika wa Bwana alimtokea akamwambia kuwa sadaka zako na sala zako zimefika
mbele za Mungu na kuwa ukumbusho. Na baada ya hapo akaambiwa akamlete mtume
Petro aje amwambie Neno la Bwana.
Nataka uone jambo hapa: kilichomsukuma Mungu kutuma malaika
kwenda kwa Kornelio ni kwa sababu ya akiba ya sadaka pampja na maombi yake
mbele za Mungu.
Kwa leo tuangalie kile kipengele cha akiba ya maombi ambayo yamekuwa
ni ukumbusho mbele za Mungu.
-
Biblia inaonyesha wazi kabisa kwamba mtu anaweza akawa
ana akiba ya maombi mbele za Mungu na Mungu akaitumia hiyo akiba kwa ajili ya
kumletea mtu huyo mssada pale atakapokuwa anauhitaji.
-
Hapa kwenye hii story hatuoni kama huyu Kornelio
alimuomba Mungu ampe msaada lakini kwa sababu sala zake zimekuwa ni ukumbusho
maana yake akiba yake ya maombi ilikuwa inadai mbele za Mungu kuwa huyu apewe
msaada hivyo ilimbidi Mungu amletee msaada.
Hebu
tuangalie mistari ifuatayo inaelezea jambo la ukumbusho wa maombi yetu mbele za
Mungu.
Ø Ufunuo 5 : 8 – vitasa vilivyojaa manukato
ambayo ni maombi ya watakatifu
Mbinguni, maombi yetu huwa
yanapimwa, na pia huwa yanakuwa ni manukato kwa Mungu maana yake yanaleta
harufu nzuri kwa Mungu mpaka yanamfanya akumbuke haja za kila mtu aliyekuwa
anaomba hayo maombi yaliyokuwa manukato.
Kwa hiyo kila akisikia harufu nzuri
ya yale manukato basi anakumbuka haja za watakatifu wake walioomba.
Ø Isaya 43 : 26 – Unikumbushe na tuhojiane, eleza
mambo yako upate kupewa haki yako
Ø Isaya 62 : 6 – 7 – Ninyi wenye kumkumbusha
Bwana msikae kimya wala msimwache akakaa kimya
Ni tabia ya
Mungu kutaka kukumbushwa juu ya haja zetu tulizomuomba mbele zake.
-
Haimaanishi kuwa Mungu amesahau bali anachotaka Mungu
ni kuona uhitaji tulionao juu ya kile tunachomuomba.
-
Ile kwamba tunaombea jambo Fulani mara kwa mara
inaonyeha ni kwa jinsi gani tunahitaji Mungu atusaidie katika jambo hilo.
-
Kwa mfano, fikiria una mtoto ambaye ni mwanafunzi na
anadaiwa ada ya shule, sasa anakuja kukuambia wewe mzazi wake. Kutoa hiyo hela
ya ada kunategemea na jinsi mtoto huyo atakavyokuambia, mwingine
atakavyokuambia utaona kuna haja ya kumpa hapo hapo au utaona haina uharaka
sana wa kuitoa hiyo ada hapo hapo. Ndivyo na kwa Mungu wetu kulivyo.
-
Unaweza ukawa unahitaji Mungu akufanyie jambo Fulani
lakini ukawa hauko serious katika kumuomba Mungu, kwa hiyo Mungu naye
akachelewa kukufanyia jambo hilo.
-
Ule u-serious unaokuwa nao kwenye maombi ndio
unaomfanya Mungu akuhudumie kwa haraka. (lakini kila jambo ni kama linaendana
na makusudi ya Mungu).
¨
Hivyo unapoomba mara kwa mara unakuwa unamkumbusha
Mungu juu ya haja zako ulizo nazo lakini utakapopita kwenye shida ambayo
itakufanya ushindwe kuomba ikupasdavyo basi yale maombi ambayo yapo kama akiba
yatasimama kama ukumbusho mbele za Bwana kwa ajili yako. Na Mungu atakuletea
msaada wa kukuvusha katika hali uliyonayo kwa sababu ya akiba hiyo ya maombi.
Na ukumbuke ya kwamba hatuachi kuomba kwa sababu jambo Fulani
tumeliombea kwa muda mrefu au kwa sababu tumechoka kuomba bali ni kwa sababu
Mungu ametenda kama tulivyomuomba au kwa sababu amani ya Kristo ndani yako
imekusukuma kuliachilia jambo hilo kwa shukrani kwa njia ya imani kuwa Mungu
atatenda kwa wakati wake kama apendavyo Yeye mwenyewe.
Kwa hiyo usione shida kuendelea kumkumbusha Mungu juu ya
mahitaji yako mbele zake.
v Kuna
mazingira unaweza ukapitia kwenye maisha yako ambayo ni magumu na yakakufanya
hata ushindwe kuomba. Sasa kama ulikuwa ni muombaji kipindi cha nyuma basi ujue
kwamba Mungu huwa anaweza kutumia akiba ya maombi yako kuja kukusaidia katika
hali hiyo unayoipitia.
Waefeso 6 :
13 – angalia lile neon analosema “mpate kushindani siku ya
uovu”
-
Siku ya uovu maana yake ni siku za shida au za hatari
au siku zenye changamoto kwa mwanadamu.
-
Na kila mtu anazo siku za uovu, maana yake kila mtu
kuna siku atapitia kwenye shida Fulani ambayo atahitaji Mungu amsaidie hata
kama yeye atashindwa kuomba. Sasa Mungu atakusaidia endapo tu kama wewe ulikuwa
ni muombaji maana yake ataangalia kwenye akiba yako ya maombi kama kuna kitu
cha kukusaidia au la.
Uko upendeleo kwa watoto wa Mungu (watakatifu) kwa sababu
maombi yao huwa hayapotei bali yanabaki kama ukumbusho kwa Mungu.
No comments:
Post a Comment