BAADHI YA SABABU ZINAZOWAFANYA WATUMISHI WA MUNGU WASHINDWE KUTUNZA MAFUTA YA ROHO MTAKATIFU NDANI YAO

Msisitizo wa somo hili ni kukusaidia kujua kwamba Mungu anataka umzalie matunda kwa kupitia karama aua huduma aliyokupa na matunda hayo yapate kukaa (maana yake yadumu)

Watumishi wengi wa Mungu wanaanzisha huduma mbalimbali lakini baada ya muda mfupi huwasikii tena au wengine wanaacha kabisa hata utumishi huo kutokana na changamoto mbalimbali wanazopitia.

Sio mapenzi ya Mungu waishie njiani, na hasa zaidi kama Mungu ndiye mwanzilishi wa huduma zao.

Mungu anataka watu wake wamzalie matunda na matunda hayo yakae maana yake yadumu. Kama ni uimbaji basi udumu, kama ni kuhubiri au kufundisha basi udumu kwenye utumishi huo na sio leo umeinuka halafu kesho umeanguka.

Ø  Yohana 15 : 2,  6 – 8, 16

-          Na kila tawi lizaalo hulisafisha ili lizidi kuzaa.

-          Hivyo hutukuzwa Baba kwa vile mzaavyo sana

-          Name nikawaweka mwende mkazae matunda na matunda yenu yapate kukaa.

Kuna kitu kinachoitwa Mafuta ya Roho Mtakatifu ambayo ni nguvu ya Mungu ndani ya mtu kwa ajili ya utumishi alionao.

-          Haya mafuta yanaweza yakaondoka kama hutajua namna ya kuyatunza ili uendelee kumtumikia Mungu kwa viwango vya Kimungu

-          Kwa lugha nyingine haya mafuta ya Roho mtakatifu yanaitwa upako.

-          Mfano, unaweza ukaongoza kipindi cha sifa halafu uwepo wa Mungu ukashuka watu wakaguswa na nguvu za Mungu wakabadilishwa maisha yao. Kule kushuka kwa nguvu za Mungu wakati unaongoza sifa ndiko kunaitwa upako. Na mara nyingi huo upako unatoka ndani ya mtu anayetumika katika utumishi husika, inawezekuwa uimbaji, kuhubiri, kufundisha, kuombea, n.k

SASA ZIKO SABABU ZINAZOFANYA WATU WAPOTEZE MAFUTA YA ROHO MT NDANI MWAO

1.     Kujisifia vipawa au karama walizonazo

Yeremia 9 : 23 – 24, 25

-          Bali ajisifuye na ajisifu kwamba anamfahamu na kumjua Mungu

-          Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake.

-          Mungu anataka tusijisifu kwa sababu ya vitu au vipawa tulivyonavyo bali tujisifu au tujivunie kwamba tunamjua Yeye.

 

Ø   Zaburi 20 : 7

-          Hawa wanataja magari na hawa farasi lakini sisi tutalitaja Jina la Bwana.

-          Huu mstari unaonyesha ni nini watu wanatumainia wanapokuwa kwenye vita lakini sisi tunatumainia Jina la Bwana

-          Imani yao ipo kwenye vitu wanavyodhani kwamba vinaweza vikawasaidia bali Biblia inatuonyesha kwamba anayemtumainia Mungu yeye atataja Jina la Bwana.

 

Ø  Mika 6 : 6 – 8

-          Ee, mwanadamu yeye amekuonyesha yaliyo mema, na Bwana anataka nini kwako ila kutenda haki, na kupenda rehema na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako.

-          Unajua watu wengi wanakimbilia kwenye utumishi bila kwanza kukaa na kumfahamu Mungu zaidi na kujua anataka wafanye nini kwenye kazi waliopewa.

-          Kwa mfano, mtu anakipaji cha uimbaji, sasa anakimbilia kuimba bila hata ya kukaa chini ya uongozi wa Mungu kwanza na kupokea maelekezo yake ndipo aingie kwenye huo utumishi badala yake anatumainia uwezo wake wa sauti na ujuzi wa kuimba.

-          Na ndio maana watu wengi wamepoteza mafuta ya Roho mtakatifu kwenye utumishi wao kwa sababu hiyo.

-          Kwa sababu ukitumia kipawa au utumishi uliopewa bila kumjua Yeye aliyekupa basi utakuwa unafanya kwa mapenzi yako badala ya kufanya mapenzi ya Mungu.

·         Hutoweza kumsikiliza Mungu

·         Hutoweza kumtii Mungu

·         Hutoweza kuenenda na Mungu

·         Ndani ya moyo wako utabeba huduma badala ya kumbeba Yesu.

Mfano wa Yesu kutenda mapenzi ya Mungu na sio mapenzi yake mwenyewe.

-          Yohana 14 : 23 – 24- nalo neon mnalolisikia silo langu ila ni lake Baba aliyenipeleka

-          Yohana 7 : 16, 17- mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka

-          Yohana 7 : 18- yeye anenaye kwa nafsi yake tu hutafuta utukufu wake mwenyewe

Mungu anapokupa huduma au karama yoyote, anachotaka ni ndani yako kuwe na utii na kusikiliza neno lake linasema nini juu ya utumishi ulionao

Ø  2Korintho 10 :  17 – 18

-          Mtu mwenye kukubaliwa si yeye ajisifuye bali ni yeye asifiwaye na Bwana

-          Watu wengi wanadhani huduma ndizo zinawapa kibali mbele za Mungu, NO, Kumjua Bwana ndio kutakakokupa kibali

 

 

2.     Kuwa na michanganyo ya kidunia

Ufunuo 3 : 15 – 18

-          Nayajua matendo yako yakwamba hu baridi wala hu moto, ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi kwa sababu una uvuguvugu, nitakutapika utoke katika kinywa changu

-          Kuwa vuguvugu maana yake ni kuwa na michanganyo yaani kwa Yesu upo na kwa shetani pia upo.

-          Mtu wa michanganyo asitegemee kabisa kuona nguvu za Mungu zikikaa ndani yake.

-          Unaweza ukabakiwa na kipawa chako lakini upako wa Mungu haupo juu yako.

Mathayo 6 : 24

-          Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.

-          Anaposema hamwezi kumtumikia Mungu na mali maana yake ni kwamba kuna namna mali inachukua nafasi ya Mungu moyoni mwako na inakutumikisha.

-          Kwa hiyo hapo unakuwa na michanganyo kwa sababu umechanganya mali na Mungu mahali pamoja.

-          Yule utakayemtumikia (Mungu au mali) ndiye atakayeachilia nguvu zake kwako

1 Yohana 2 : 15 – 17

-          Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

 

SIFA/ VIASHIRIA (INDICATORS) VYA WATUMISHI WA MUNGU WALIOPOTEZA MAFUTA YA ROHO MTAKATIFU NDANI YAO:-

1.      Hawana hofu ya Mungu ndani yao

-          Warumi 1 : 28 – 32

-          Na kama walivyokataa kuwa na mUngu kwenye fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa

 

2.      Ni watu wasiojishusha au wasiojinyenyekeza mbele za Mungu

-          Sio watu wanaotaka tena kuongozwa na Mungu, wanataka kujiongoza wenyewe.

-          Yohana 14 : 23 – 24mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu

-          1Petro 5 : 6Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Bwana...

 

3.      Ni watu wanaotii huduma zaidi kuliko kumtii Mungu

-          1 Samweli 15 : 1 – 3, 9, 10 – 11, 19 – 23

-          Mbona basi hukutii sauti ya Bwana, bali ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana?

 

4.      Hawana muda wa kutosha wa maombi na Mungu wao

-          Wanaamini katika uwezo wa vipawa na huduma zao

-          Hakiwasumbui kama Mungu yupo pamoja nao au hayupo nao kwenye utumishi wao

-          Kutoka 33 : 15 – 16

 

5.      Hawana muda wa kutosha wa kusoma na kutafakari neno la Mungu

-          Yoshua 1 : 8- kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako bali utafakari mchana na usiku, ukaangalie kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo, maana ndipo utakapoifanikisha njia yako kasha ndipo utasitawi sana

-          Zaburi 119 : 11 – moyoni linakaa Neno la Kristo

 

NB: Ukiskosa neno la Kristo ndani yako maana yake umekosa kuwa na imani kwa sababu imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia kunatokana na Neno la Kristo (Rumi 10 : 17). Na kama hauna imani ndani yako huwezi ukampendeza Mungu kwa sababu kila amwendeaye Mungu ni lazima aamini kwamba yupo (Ebrania 11 : 6). Na jambo lolote lifanyikalo bila imani hilo ni dhambi (Rumi 14 : 23b)

-          Kwa hiyo ukikosa neno la Mungu ndani yako ni lazima tu utatenda dhambi

 

6.      Wanamwabudu Mungu kwa mazoea

-          Mathayo 15 : 8

-          Wanamwabudu Mungu kwa midomo tu bali mioyo yao ipo mbali naye

-          Maana yake wanamwabudu kimazoea.

 

7.      Hawana uvumilivu ndani yao juu ya ahadi za Mungu kwenye utumishi walionao

-          1Petro 5 : 6

-          Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari ili apate kuwakweza kwa wakati wake

-          Tafsiri ya neno kuwakweza maana yake ni kuwapandisha au kuwainua.

-          Na pia Biblia inasema apate kuwakweza kwa wakati wake na sio kwa wakati wako.

-          Mungu anajua muda sahihi wa wewe kuinuka kihuduma. Kuna wakati anajua kabisa kwamba ukifika level Fulani hutaweza kusimama vizuri na Yeye kwa sababu inawezekana kuna misingi bado hujaiweka imara kusimama kwenye level hiyo.

-          Kwa hiyo Mungu anachotaka ni wewe uendelee kumfahamu Yeye zaidi na zaidi na zaidi ili ukue zaidi.

No comments:

Post a Comment

Katika maisha yako usisikilize watu wanasema nini bali msikilize Mungu anasema nini, kwa sababu watu hawajui ni nini ambacho Mungu amekupang...