DARASA LA KUUKULIA WOKOVU
Karibu tena katika darasa la
kuukulia wokovu, na leo tunaangalia zaidi katika mambo yanayotokea au kufanyika
mara tu unapookoka.
Tunaokolewa kwa neema ya Mungu wa
si kwa matendo yetu – Waefeso 2 : 8
-
Wokovu wetu hautokani na matendo yetu mazuri
wala hadhi tulizonazo katika ulimwengu huu bali ni neema ya Mungu ndiyo
inayotupa nafasi ya kuokolewa.
Kuna mambo yanatokea pale tu mtu anapookoka:
1.
Unasamehewa
dhambi zako zote.
Ø Isaya 43 : 25 – Mimi ndimi niyafutaye
makosa yenu kwa ajili yangu wala sitazikumbuka dhambi zenu.
Ø 1 Yohana 1 : 9 – tukiziungama dhambi
zetu, Yeye ni mwaminifu hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu
wote
Ø 1 Yohana 1 : 7- damu ya Yesu
inatusafisha dhambi zote
Hiyo ni baadha ya mistari
inayoonyesha kuwa Mungu anatusamehe dhambi zetu zote, anazifuta zote. Kwa hiyo
ndani yako usije ukaanza kjikumbushia maisha yako ya kale, unaweza ukajiona
kama bado hujasamehewa.
2.
Jina
lako linaandikwa kwenye kitabu cha uzima kule mbinguni.
Ø Ufunuo 20 : 15 – na iwapo mtu yeyote
hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la
moto
Ø Luka 10 : 20 – furahini kwa sababu
majina yenu yameandikwa mbinguni
Jina lako kuandikwa mbinguni
maana yake ni kwamba mbingu zinakutambua, unajulikana mbinguni.
3.
Unapata
nafasi ya kuwa mwana familia katika familia ya Mungu (katika ufalme wa Mungu)
Ø Waefeso 2 : 19 - nyinyi si wgeni wala
wapitaji bali watu wa nyumbani kwake Mungu
Ø Wakolosai 1 : 13 – akatuokoa
akatuhamisha katika ufalme wa Mwana wa pendo Lake.
Hapo mwanzo ulikuwa huna ushirika
na Mungu lakini baada ya kuokoka Mungu anakuwa baba yako na wewe unakuwa kwake
Mwana.
Unakuwa na haki ya kuwa mtoto wa
Mungu
Ø Yohana 1 : 12 – bali wote waliompokea
aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu
Ø Mathayo 6 : 9- biblia inasema “Baba ytu
uliye mbinguni” haisemi Mungu wetu uliye mbinguni.
Hii inaonyesha wazi kwamba
tumefanyika watoto wa Mungu.
4.
Unapata
ukombozi mbali na kila kilichokufunga kwenye maisha yako.
Ø Wakolosai 1 : 13 – Naye alituokoa
kutoka katika nguvu za giza – tafsiri yake ni kwamba alituokoa kutoka kwenye
vifungo na mateso ya Ibilisi.
Ø Waefeso 1 : 7 – msamaha wa dhambi ni
sawa sawa na ukombozi
Kwa hiyo unaposamehewa dhambi
zako, Mungu anakuweka mbali na mateso na uonevu wa kila aina wa shetani.
5.
Unapewa
mamlaka ya kiutawala katika ulimwengu war oho
Ø Waefeso 1 : 20 – 22 & Waefeso
2 : 6 – Tumeketishwa eneo la juu sana la mamlaka katika ulimwengu wa roho.
Tumeketishwa pamoja na Kristo Yesu.
Ø Ufunuo 5 : 9 – 10 – Tulinunuliwa kwa
damu ya Yesu tukafanywa kuwa wafalme na makuhani kwa Mungu
Hizo zote zinaonyesha nafasi za
kiroho tunazozipata tukishaokoka.
Na kila nafasi ina majukumu yake.
6.
Mwili
wako unakuwa ni hekalu la Roho Mtakatifu (pia wewe mwenyewe unakuwa mtakatifu)
Ø 1 Wakorintho 3 : 16 – 17 – miili yetu
imkuwa ni hekalu la Mungu, na Roho wa Bwana anakaa ndani yetu.
Ø 1 Petro 1 14 – 16 - mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni
mtakatifu.
Tunapookoka, miili yetu inakuwa
si mali yetu wenyewe bali ni mali ya Bwana, hivyo tunatakiwa tuishi kwa kuepuka
uovu.
KWA NINI NI LAZIMA KUOKOKA?
Tunaokoka ili:
a. Ili
tupate uhakika wa kuingia katika uzima wa milele
b. Ili
tupate baraka na ahadi za Mungu katika maisha yetu
c. Ili
tusiwe watumwa wa nguvu za giza
No comments:
Post a Comment