Msisitizo wa somo hili ni kukujengea msingi imara wa kumtegemea Mungu katika hali zote bila kutetereka.
Somo hili litakusaidia kutengeneza msingi imara wa kumtegemea
Mungu kwa kiwango kinachohitajika mbele zake
bila kujali mazingira unayopitia
Zaburi 27 :
1 – 3
“Bwana ni nuru yangu na wakovu wangu nimwogope nani?”
Kuna mambo mawili ninayoyaona katika mistari hii: (i) kuna watu wanakuwa na hofu ndani
mwao japo Mungu wao ni ngome na wokovu wao (ii)
kuna watu ile hofu inapotea pale wanapojua kuwa Mungu ni ngome na wokovu wao.
Mithali 3 : 5 inasema “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote wala
usizitegemee akili zako mwenyewe”.
-
Nataka ufahamu jambo hili, kwamba unapopitia kwenye
shida au mazingira yoyote magumu kwenye maisha
yako halafu ndani yako ukajawa na hofu basi ujue kiwango chako cha
kumtegemea Mungu kimepungua.
-
Kumtegemea Mungu ni jambo la imani kwa sababu
imeandikwa (Ebrania 11 : 6) kwamba amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yupo.
Hivyo tunaposema kiwango chako cha kumtegemea Mungu kimepungua maana yake ni
kuwa kiwango chako cha imani juu ya Mungu wako kimepungua.
Maandika yanasema tunatoka imani hata imani (Warumi 1 : 17). Hii inadhihirisha wazi
kuwa imani ina viwango. Pia ina maana kuwa imani inaweza kuongezeka au
kupungua.
Mfano 1:
Mathayo 17 : 14 – 21 na Marko 9 : 37 – 42
Imani aliyokuwa anaiongelea Yesu sio imani ya kumjua Mungu
bali ni imani ya kuwasaidia kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo. Yesu alikuwa anawaambia kuwa kumwamini Yesu
anayeweza kuwaokoa na dhambi ni tofauti na kumwamini Yesu anayeweza kuwaokoa na
magonjwa.
-
Unaweza ukawa na Yesu ambaye ni Mkombozi wako lakini
ukawa huna Yesu ambaye ni Mponyaji.
-
Kwa hiyo fahamu kwamba kiwango chako cha imani
kikipungua basi ujue kuwa kuna aina ya changamoto ukizipitia nhutoweza
kuzishinda. Hii ni kutokana na kwamba kila changamoto inayokutana nayo
inahitaji level Fulani ya imani ili uishinde hiyo changamoto.
Yesu alikuwa anawaambia kuwa kilichowafanya mshindwe kutoa pepo
Yule si kwa sababu hamniamini mimi bali ni kwa sababu ndani yenu kuliingia hofu
ikapunguza kiwango cha imani yenu juu ya nguvu za Mungu za kuponya.
Waefeso 3 :
20 “Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo makubwa mno kuliko
yale tuyaombayo au tuyawazayo kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu”.
-
Neon “kwa kadiri” maana yake “kwa kiwango”. Kwa hiyo
utendaji kazi wa Mungu kwenye maisha yako unategemea kiwango cha nguvuya Mungu
inayotoka ndani yako, nguvu hiyo inaachiliwa kwa nia ya imani.
-
Hiyo imani ikipungua na nguvu ya Mungu inayoaachiliwa
ndani yako nayo inapungua.
NB: Hofu ni
adui mkubwa sana wa imai yako. Na upate kujua ya kwamba huoweza kuvuka kwenye
mazingira yako kama hofu inayokuzuia haijaondoka ndani yako.
Kazi ya
hofu ni ku-disconnect nguvu ya Mungu iliyopo ndani yako isishughulike na tatizo
ulilonalo.
Mifano
mingine zaidi:
Ukisoma Mathayo 9 : 29 – ndipo alipowagusa
macho yao akasema kwa kadiri ya imani yenu mpate.
Maana yake
ni kwamba unpokea kwa Bwana kwa kadiri ya imani yako.
Pia ukisoma
Luka 10 : 17 – ndipo wale sabini
waliporudi kwa furaha wakisema hata pepo wanatutii kwa jina lako
NAMNA YA KUSHUGHULIKIA HOFU ILIYOPO NDANI YAKO
1.
Kusoma Neno
la Mungu kila wakati
Kuwa na tabia ya kusoma Neno la Mungu mara kwa mara kutakusaidia
kukujengea uhakika wa kumjua Mungu na nguvu zake. Hivyo utafahamu kuwa hakuna
lisilowezekana kwa Bwana.
Kumb 20 : 1
– 4 – kila wakati Yesu atakuambia usiogope kwa maana yeye yuko
pamoja na wewe ili akuokoe.
Kwa kupitia Neno la Mungu unaifahamu kweli ya Mungu.
2.
Kufunga na
kuomba
Mathayo 17
: 21 – namna hii haitoki isipokuwa kwa kufunga na kuomba. Hapa
Yesu haongelei kwamba uombe ili utoe pepo au uponye bali anatuelezea kuwa na
tabia ya kuwa na maombi ya mara kwa maraitaondoa hali ya kutokuamini ndani
mwako.
Kinachokwamisha watu wasione matokeo ya kile wanachokiomba
sio nguvu za Mungu bali ni kiwango cha nguvu hizo za Mungu zinazotoka ndani
yako.
3.
Kuhudhuria
ibada mara kwa mara
1
Wathesalonike 5 : 11 na Yuda 1 : 20
Biblia inasema “Basi farijianeni na kujengana kila mtu na
mwenzake.” Pia mahali pengine anasema “Bali ninyi wapenzi mkijijenga juu ya
imani iliyo takatifu sana na kuomba katika Roho
Mtakatifu”.
Kuhudhuria katika ibada ni agizo la Bwana wetu Yesu Kristo
nani njia pekee ya kujengna kiimani kwa sababu imani ni kama mkaa usiowaka moto
lakini ukiuchanganya na mikaa mingine inayowaka moto basi hata ule usiowaka
moto nao utawaka moto.
No comments:
Post a Comment