Mathayo 5 : 14 – 16
Yohana
9 : 5 – Yesu ni nuru ya ulimwengu
(Mathayo 6 : 1- Angalieni msifanye wema
wenu machoni pa watu kusudi mtazamwe na wao, kwa maana mkifanya kama hayo,
hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni)
NB: Biblia inatufundisha mambo kadhaa hapa
kutokana na hii mistari
1.
Biblia inatutambulisha sisi ni akina nani.
Ninyi ni nuru ya
ulimwengu.
2. Pia Bblia inatujulisha
kazi au wajibu tulionao kutokana na utambulisho tulio nao
Nuru yenu na iangaze mbele
ya watu.
3. Na mwisho Biblia
inatujulisha nini kinatokea tunaposimama kwenye nafasi zetu vizuri
Wapate kuyaona matendo mema,
wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni
Yesu Kristo katika hotuba yake ya mlimani
anaweka msingi wa kanisa kama chombo muhimu cha kuuleta ufalme wa Mungu
duniani.
-
Watu walidhani amekuja kutengua
torati bali kumbe amekuja kutimiliza.
-
Kuna maeneo ya torati yaliwekwa
kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya waisraeli kipindi wanatoka nchi ya Misri
wakielekea Kanaani.
Baadhi ya maeneo aliyoyagusia Yesu katika
hotuba yake ni kama ifuatavyo:
-
Mathayo 5: 21, 22, 23
-
Mathayo 5: 27, 28
-
Mathayo 5: 33, 34
-
Mathayo 5: 38, 39
-
Mathayo 5: 43, 44 – 48
-
Na maeneo mengine
Mathayo
5 : 20
Haki yenu isipozidi haki ya mafarisayo,
hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni
-
Hii inamaanisha kwamba kuna
maisha unaweza ukaishi ukidhani kuwa upo tofauti na watu amabao hawajaokoka lakini kumbe hauna
tofati nao.
-
Ndio maana anasema haki yenu
lazima izidi haki ya mafarisayo
Kwa mfano, mtu
akikukosea wewe uliyeokoka na mtu akimkosea mtu ambaye hajaokoka, tofauti yenu
itaonekana wapi?
-
Itaonekana kwenye kupokea
maudhi hayo (reaction)
-
Pia itaonekana kwenye eneo la
kusamehe (muda utakaochukua kusamehe na
sababu zitakazokufanya usamehe)
No comments:
Post a Comment