Katika maisha yako usisikilize watu wanasema nini bali msikilize Mungu anasema nini, kwa sababu watu hawajui ni nini ambacho Mungu amekupangia bali wanaona kile kinachotokea kwa wakati ule wanapokuona, hawajui yakuwa kuna mipango mizuri ambayo Mungu amekupangia mbele ya maisha yako. Yeremia 29:11
"nayajua mawazo ninayowawazia si mawazo mabaya bali ni ya mema ya kuwapa tumaini katika siku zenu za mbele".
pia kumbuka kuwa kile unachokisikia na kukiamini ndicho kinachotokea kwenye maisha yako. Isaya 53:1
"nani aliyesadiki habari tulizozileta, na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?"
Kwa hiyo ni muhimu kujifunza kumsikiliza Mungu na sio wanadamu.
Mwanadamu ameumbwa kwa namna ambavyo anaona vitu vya wakati huu tu, hivyo mawazo yake yanatokana na kile anachokiona. ndani ya kila mwenye imani katika Kristo anaouwezo wa kuona hata mambo ya sirini (yaani mambo yaliyositirika ya baadae). Huyu mtu anauwezo wa kujua mawazo ya Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu na akaishi kwa kufuatana na ile mipago na mawazo ya Kimungu. ukiishi katika ramani ya Mungu aliyokupangia utakuwa ni mshindi katika kila hatua kwa sababu ndani yako utakuwa unajua ni nini cha kufanya kwa wakati upi, na pia utajua aina tofauti tofauti ya vipindi katika maisha yako kwa sababu tayari ndani yako unayo picha halisi ya maisha yako (tayari unajua mwanzo wako na mwisho wako kwa njia ya huyo Roho Mt. kwa maana yeye mwenyewe amesema atatujulisha mambo yatakayo kuja).
Ni maombi yangu kwamba unastahimili yote na kuyashinda yote kwani ushindi tayari upo ndani yako.
Yaheshimu na uyatunze maisha uliyopewa na Mungu, maana maisha yako ni ya thamani sana kuliko kitu chochote ulichonacho. kumbuka kwamba kesho yako inatengenezwa leo, na pia ukiwa kama kijana inawezekana kujitunza na kulinda heshima aliyokupa Mungu.
You are so Precious than Gold.

UJUMBE WA LEO

Silaha hutengenezwa wakati wa amani japo hutumika wakati wa vita.
wakristo wengi wakati wa amani hawaombi ila mambo yakibadilika kidogo hufunga na kuomba na muda huo mambo yanakuwa yameharibika.

Katika maisha yako usisikilize watu wanasema nini bali msikilize Mungu anasema nini, kwa sababu watu hawajui ni nini ambacho Mungu amekupang...